Ukame unatishia Maisha ya Wafugaji.

Na Baraka Ole Maika;

Hali ya Ukame unaendelea kuwa tishio kwa maisha ya Wafugaji na Mifugo yao Katika Wilaya ya Longido,Monduli Mkoani Arusha na Simanjiro Mkoani Manyara.

Kutokana na Ukosefu wa Majani Jamii hiyo ya Wafugaji wameanza kuhama na Mifugo yao kuelekea Maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga kwa ajili ya Malisho na Maji ili kunusuru Mifugo yao ambao ndio njia kuu ya Uchumi wao.

Aidha hali hiyo ya Ukame umewapelekea Wafugaji kununua Pumba ya Mahindi na Mazao Mengine kwa Gharama ya Tsh 23,000 hadi 35,000 kwa Gunia la Kg 100 na kuwalisha baadhi ya Mifugo wao ambao wamedhoofika na kushindwa kwenda malishoni.

Hali hiyo ya Ukame unatishia hali ya Mifugo na Maisha ya Wafugaji kwa kuhofia kuwapoteza Mifugo yao kwa Wingi endapo Mvua haitanyesha kuanzia sasa hadi Mwezi Novemba.

orkonerei

Location: Simanjiro-Manyara Frequency: 94.4 Mhz Contact: Tel: +255 787 507 854 or +255 769 712 961 Orkonerei Radio Servce(ORS Fm 94.4) ni Radio ya Jamii iliyoanzishwa na Taasisi ya Kijamii ya Ilaramatak Lorkonerei(Institute for Orkonerei Pastoralists Advancement-IOPA) katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara June 2002 ikiwa na Lengo la Kutetea na Kuhamasisha Jamii ya Wafugaji katika Shughuli za Maendeleo na kuwajengea Ufahamu na Uelewa kupitia Upashanaji wa Habari katika nyanja ya Elimu,Afya,Mazingira,Jinsia,Uchumi,Mifugo,Kilimo,Uongozi na Utawala Bora.

Leave a Reply