WATOTO WOTE WAPEWE ELIMU SAWA

Na Habiba Mpimbita

Wananchi wa Mkoa wa Mtwara na wilaya zake wametakiwa kuachana na mawazo mgando ya kuwabagua watoto kijinsia katika suala la utoaji wa elimu ili kuwajengea misingi bora watoto wao.

Hayo yamesemwa na Afisa elimu, vifaa na takwimu wa Wilaya ya Mtwara vijijini Bw. Kitonka Manase na kuwahasa wazazi kutowanyima haki ya msingi ya kupata elimu watoto wa kike kwa sababu za kimila na desturi.

Aidha Bw.Manase amewaomba Wasichana waliofanikiwa katika elimu kuwasaidia wasichana ambao bado wapo kwenye adha hii na jamii kwa ujumla kwa kuwapa elimu ili waeze kubadilika kifikra,na kuongeza kuwa sheria haibagui jinsia,dili ,wala kabila.

Na kwa upande wake Lenfrida Mwagama Mwanafunzi wa chuo cha kilimo mkoani Mtwara,amewashauri wasichana ambao wamepata nafasi ya kupata elimu waitumie vizuri ili iwasaidie kujiajiri wenyewe katika maisha yao na si kuajiriwa.


Hata hivyo nchini Tanzania takwimu zinaonyesha tatizo la ubaguzi wa kijinsia katika utoaji wa elimu kwenye miaka ya hivi karibuni kutokana na jitahada zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo elimu zinazoendelea kutolewa kwa wananchi,ikiwa kwa Mwaka 2012 takwimu zinaonyesha uwiano sawa kati ya wasichana na wavulana katika elimu ya msingi,katika elimu ya sekondari ya kawaida uwiano ni 0.6% na sekondari ya juu ni 0.5%,hali inayoashiria kupungua kwa uwiano huo ukilinganisha na mwaka 2017 ambapo uandikishaji katika elimu msingi wavulana milioni 4629027 sawa na 49.7% wasichana milioni 4688383 sawa 50.3% katika jumla ya wanafunzi milioni 9317410 na kwa upande wa sekondari jumla ya wanafunzi 199019 wameandikishwa ikiwa wavulana 947,486 sawa 49.6% na wasichana 961,531 sawa 50.4%.

Jamii Fm Radio

Jamii Fm Radio

Location: Naliendele- Mtwara Frequency: 90.5 MHz Contact: jamiifmradio90.5@gmail.com mtukwaomedia@yahoo.co.uk +255712087580, +255782510474, +255685307828 Jamii FM Radio is a community radio that intends to operate its radio station pursuant to non commercial. The main objective is to raise discussion about issues that are important to the people in rural communities in the Mtwara and Lindi regions. Jamii FM Radio wants to offer people on the grassroots level a possibility to take part in the public debate about issues concerning their livelihoods, about alternative ways of development and through this process a chance to find the best possible solutions to the development of their local areas in order to advance democracy, human rights and good governance. Jamii fm ni kituo cha radio ya kijamii yenye lengo la redio kusaidia kupaza sauti za wanajamii hasa waishio vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa maendeleo kupitia majadiliano. Jamii Fm Radio inasaidia wananchi kuibua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa, kuhusu aisha yao, maendeleo yao, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. KARIBU SANA MTWARA-TANZANIA WELCOME MTWARA-TANZANIA

Leave a Reply