WANANCHI WA MKOA WA MTWARA NA MIKOA JIRANI WAMEHASWA KUTUMIA FURSA YAKIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA COMORO ILI KUIMARISHA UCHUMI

Na Amua Rushita,

Chama cha Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA)wamesaini hati ya makubaliano ya kibiashara na ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro kupitia Chama cha Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo nchini humo(UCCIA).
Hafla ya makubaliano hayo yamefanyika mkoa hapa kwa ujumbe wenye wawakilishi saba wa vyama vya wafanyabiashara viwanda na kilimo kutoka Comoro na visiwa vyake vidogo vya Ngazija, Hanjuani .

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah amesema ni fursa kwa wafanyabiashra wa Mtwara kuuza bidhaa zao nchini Comoro kwani kiwango cha mauzo ya Tanzania kwa sasa ni asilimia 0.53 kiasi ambacho ni kidogo sana kulingana na ukaribu wetu, na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2020.

Swallah ameweka wazi mikakati ya chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara kuhusu kuimarisha huduma za kibiashara baina ya Comoro na Tanzania na kuwaasa wananchi kuitumia Meli mpya ambayo itaanza safari zake Januari 2018.

Naye Rais wa Chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo nchini Comoro (UCCIA) Ahmed Ali Bazi amesema wameamua kuja kusaini makubaliano Mkoani Mtwara kwasababu ni karibu sana na nchi yao na kuna bidhaa nyingi ambazo wao wanazihitaji kama ambavyo wameanza kupata cement lakini bado wanahitaji zaidi vyakulana na bidhaa zingine.

Mfanyabiashara kutoka Mtwara Fadhiri Bashir ambae wamenunua meli kwa kushirikiana na mfanyabiashara kutoka Comoro ili kuimarisha biashara, kwani Meli ya awali ambayo inaendelea kufanya kazi ni ndogo ukilinganisha na huhitaji wa bidhaa kutoka Mtwara kwenda visiwa vya Comoro na Meli hiyo itatatua tatizo la uhaba wa usafirishaji, na itaanza kufanya kazi mwezi wa kwanza January 2018 na itafanya safari kwenda msumbiji, Tanzania na Comoro.

Biashara baina ya nchi hizi mbili kupitia Bandari ya Mtwara ulianza rasmi mwezi August mwaka huu na uzinduzi huo ulifanywa na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego na pia Balozi wa Comoro nchini Tanzania.

Jamii Fm Radio

Jamii Fm Radio

Location: Naliendele- Mtwara Frequency: 90.5 MHz Contact: jamiifmradio90.5@gmail.com mtukwaomedia@yahoo.co.uk +255712087580, +255782510474, +255685307828 Jamii FM Radio is a community radio that intends to operate its radio station pursuant to non commercial. The main objective is to raise discussion about issues that are important to the people in rural communities in the Mtwara and Lindi regions. Jamii FM Radio wants to offer people on the grassroots level a possibility to take part in the public debate about issues concerning their livelihoods, about alternative ways of development and through this process a chance to find the best possible solutions to the development of their local areas in order to advance democracy, human rights and good governance. Jamii fm ni kituo cha radio ya kijamii yenye lengo la redio kusaidia kupaza sauti za wanajamii hasa waishio vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa maendeleo kupitia majadiliano. Jamii Fm Radio inasaidia wananchi kuibua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa, kuhusu aisha yao, maendeleo yao, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. KARIBU SANA MTWARA-TANZANIA WELCOME MTWARA-TANZANIA

Leave a Reply