Ifahamu Jamii fm

Utangulizi
Jamii FM Radio, ilianza matangazo yake rasmi mwezi Septemba mwaka 2016. Madhumuni ya Radio hii ni kupasha Habari na kutoa fursa ya Mawasiliano kwa Jamii, hasa Jamii ya vijijini. Vipindi vyake vinaandaliwa kwa namna inayogusa na kulenga maisha ya jamii ya vijijini, ikiwa ni pamoja na watu wenye mahitaji maalum kama Walemavu na watu wasiojiweza.

Radio Jamii FM hutangaza habari zinazoelimisha na kuwa Jukwaa la kubadilishana habari za maendeleo ya jamii, hivyo kutengeneza fursa huru kwa jamii kupaaza sauti. Ushirikishwaji jamii unasisitizwa katika kuandaa vipindi. Hivyo,Radio Jamii hutoa fursa kwa wasio na sauti katika Jamii kupaza sauti.

Dira
Kuona kwamba kupitia Radio Jamii FM, Jamii ya Mikoa ya Mtwara na Lindi hasa inayoishi vijijini, inapata habari na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazohusu maendeleo yao.

Dhima
Kuwezesha Jamii kutumia Vyombo vya habari katika kukuza mawasiliano shirikishi ili kujiletea maendeleo endelevu

Eneo
Kituo cha Radio Jamii kipo Kitongoji cha Naliendele, kilichopo umbali wa kilometa 9 kutoka Mtwara Mjini katika barabara inayoelekea Newala. Kituo hiki kipo mkabala na Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo, Naliendele, Mtwara

Eneo la Huduma
Radio Jamii inamiliki Mnara wenye urefu wa Mita 60 unaowezesha Kituo kurusha matangazo na kufikia idadi kubwa ya wakazi wa eneo hili kuanzia Manispaa ya Mtwara na kusambaa hadi kufikia Nanyamba, Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea, Lindi na baadhi ya maeneo yanayoambaa kwenye mpaka wetu na Nchi jirani ya Msumbuji

Tembelea kwenye website yetu kwa kubonyeza Hapa

Jamii Fm Radio

Jamii Fm Radio

Location: Naliendele- Mtwara Frequency: 90.5 MHz Contact: jamiifmradio90.5@gmail.com mtukwaomedia@yahoo.co.uk +255712087580, +255782510474, +255685307828 Jamii FM Radio is a community radio that intends to operate its radio station pursuant to non commercial. The main objective is to raise discussion about issues that are important to the people in rural communities in the Mtwara and Lindi regions. Jamii FM Radio wants to offer people on the grassroots level a possibility to take part in the public debate about issues concerning their livelihoods, about alternative ways of development and through this process a chance to find the best possible solutions to the development of their local areas in order to advance democracy, human rights and good governance. Jamii fm ni kituo cha radio ya kijamii yenye lengo la redio kusaidia kupaza sauti za wanajamii hasa waishio vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa maendeleo kupitia majadiliano. Jamii Fm Radio inasaidia wananchi kuibua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa, kuhusu aisha yao, maendeleo yao, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. KARIBU SANA MTWARA-TANZANIA WELCOME MTWARA-TANZANIA

Leave a Reply