Mbunge wa Mtwara Mjini alilia ondoleo la Kodi (VAT) kwenye taulo za kike (Pedi)

Mbunge wa Mtwara mjini Mh Maftah Nachuma kupitia chama cha wananchi CUF, amewaomba serikali kuondoa kodi katika taulo za kike ili kuweza kuwapa kipaumbele wasichana kuhuduria masomo yao vizuri
Akichangia hoja kwenye Bunge la Bajeti leo Bungeni Jijini Dodoma, Mh Mafutaa ameomba serikali iondoe tozo katika taulo za kike na wanafunzi wapatiwe bure taulo za kike hii itasaidia sana wanafunzi hao kuwa na mahudhurio mazuri darasani.
mh-maftaha-nachuma-akizungumza-bungeni-leo-june-19-2019
Pamoja na pongezi nyingi kwa serikali kuhusu kuanzisha kituo cha uchenjuaji madini ameomba serikali kuwekeza katika elimu kwa vijana wa kitanzania katika kupata Elimu juu ya gesi na Biashara ya gesi ili kuweza kukusanya mapato badala ya kuwaachia wageni wawe katika sekta hiyo.

Amesisitiza kuwa serikali inakosa fedha katika nyingi katika sekta ya gesi na kuomba shughuli za usambazaji wa gesi uanze Tanzania kwanza kabla ya kusambaza katika nchi za nje. Katika kuhitimisha hoja yake bungeni ameomba serikali kuuza korosho kwakuwa zimeanza kuharibika wakati bado ziko gharani. sikiliza sauti yake hapa

Jamii Fm Radio

Jamii Fm Radio

Location: Naliendele- Mtwara Frequency: 90.5 MHz Contact: jamiifmradio90.5@gmail.com mtukwaomedia@yahoo.co.uk +255712087580, +255782510474, +255685307828 Jamii FM Radio is a community radio that intends to operate its radio station pursuant to non commercial. The main objective is to raise discussion about issues that are important to the people in rural communities in the Mtwara and Lindi regions. Jamii FM Radio wants to offer people on the grassroots level a possibility to take part in the public debate about issues concerning their livelihoods, about alternative ways of development and through this process a chance to find the best possible solutions to the development of their local areas in order to advance democracy, human rights and good governance. Jamii fm ni kituo cha radio ya kijamii yenye lengo la redio kusaidia kupaza sauti za wanajamii hasa waishio vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa maendeleo kupitia majadiliano. Jamii Fm Radio inasaidia wananchi kuibua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa, kuhusu aisha yao, maendeleo yao, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. KARIBU SANA MTWARA-TANZANIA WELCOME MTWARA-TANZANIA

Leave a Reply