JAMII INAWASAIDIAJE WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Wanachi wa kijiji cha Namindondi kilichopo kwenye kata ya Madimba kwenye halmashauri ya Mtwara, wamezungumza namna pekee jamii yao inavyowathamini watu wenye ulemavu na kushirikiana nao pasipokujali tofauti zao za kimaumbile na rangi za ngozi.

Muaandaaji wa kipindi amepata nafasi ya kukutana na Ndugu Hassani ameeleza namna anavyomchukulia mlemavu katika jamii yake na namna anavyotoa msaada kwa walemavu pia amekiri kuwepo kwa mazingira magumu katika jamii.

Ndugu zainabu abdalah mpilikene ambae ni mlemavu wa ngozi yeye anaeleza kuhusiana na suala la mikopo amabyo hadi hivi sasa hawajapata mikopo hio kutoka serikalini.

Pia ameaimbia jamii fm kuwa anaishi katika mazingira salama ambayo si hatarishi ya kuwindwa kama inavyofanyika mikoa ya watu wengine ile hali ya kuwepo kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wangozi kwa maana ya alubinism.

Sambamba na hayo amesema kuwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wanaishi vijijini hawapati huduma ya mafuta pamoja na sabuni ambzo zinasidia kulinda ngozi zao hivo na kuuomba msaada kwa serikali iwasaidie msaada wa mafuta na sabuni kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Mzee Issa Bin Amri Saidi ameeleza hali ambayo anayo kwasasa ya ulemavu na Maumivu ambayo anayopitia pia mtu ambae anampa msaada kwa wakati wote pia ameeleza namna anavyochukuliwa katika jamii kiujumla pamoja na hayo kazungumzia kipaumbele ambacho anapewa pale aendapo hospitali lakini pia ameomba msaada kutoka kwa serikali msaidie msaada wowote ule.

Mwenyekiti wa kijiji cha Namindondi yeye ameeleza vipaumbele ambavyo wanatoa dhidi ya walemavu pia ameeleza kuwepo kwa mazingira wezeshi ambayo yapo dhidi ya watu wenye mahitaji maalum pia ameomba jamii isiwafiche watu wenye mahitaji maalum au walemavu.
SIKILIZA KIPINDI HICHO

Jamii Fm Radio

Jamii Fm Radio

Location: Naliendele- Mtwara Frequency: 90.5 MHz Contact: jamiifmradio90.5@gmail.com mtukwaomedia@yahoo.co.uk +255712087580, +255782510474, +255685307828 Jamii FM Radio is a community radio that intends to operate its radio station pursuant to non commercial. The main objective is to raise discussion about issues that are important to the people in rural communities in the Mtwara and Lindi regions. Jamii FM Radio wants to offer people on the grassroots level a possibility to take part in the public debate about issues concerning their livelihoods, about alternative ways of development and through this process a chance to find the best possible solutions to the development of their local areas in order to advance democracy, human rights and good governance. Jamii fm ni kituo cha radio ya kijamii yenye lengo la redio kusaidia kupaza sauti za wanajamii hasa waishio vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa maendeleo kupitia majadiliano. Jamii Fm Radio inasaidia wananchi kuibua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa, kuhusu aisha yao, maendeleo yao, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. KARIBU SANA MTWARA-TANZANIA WELCOME MTWARA-TANZANIA

Leave a Reply