Makala haya yanaangazia masuala ya gesi na mafuta katika kijiji cha Madimba, Kata ya Madimba Mkoani Mtwara ambapo ndani yake ndipo kuna kiwanda cha kuchakata gesi cha TPDC kilichopo eneo la mchepa.
Nimezungumza na wananchi wa kijiji hicho ili kujua wana uelewa gani kuhusu gesi na mafuta na kujua utofauti kati ya gesi na mafuta.
Wananchi hao wanaonekana hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala hayo ya gesi na mafuta na wengi wanaonekana hawana mazoea ya kuhoji kuhusu masuala hayo.
Kipitia makala haya utafahamu faida inayotokana na uwekezaji huu pamoja na huduma za jamii wanazofaidika nazo ikiwa nia pamoja na kuatiwa huduma ya maji, Gari la wagonjwa hasa pale linapohitajika kumuwahisha mgojwa kwa wakazi wa kijiji cha madimba mkoani hapa.