AMCOS Naliendele wamegomea kusomewa makisio ya Mapato na Matumizi

Wanachama wa Chama Cha Kidogo Cha Ushirika (AMCOS) Naliendele wamegomea kusomewa makisio ya mapato na matumizi ya msimu ujao wa korosho 2019/2020 baada ya kudai kuwa idadi ya wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu maalum hawajakidhi akidi ya kikao.

Kikao hicho kilichoitishwa na ofisi ya mrajisi ambae amewakilishwa na Afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Ndg Hamidu Ndago, ambae alipata wakati mgumu kuwashawishi wanachama na wajumbe wa mkutani huo wapitishe makisio hayo ya mapato na matumizi kwa msimu ujao ila hali ilikuwa ngumu.

Baadhi ya wanachama walianza kutoa maoni yao kwanini hawataki kupitisha makisio ya mapato na matumizi, huyu hapa Ahmad Issa Chihipu anaeleza.

Nae Said Seleman Amezungumzia Kuhusu Kutokubali Kupitisha Mapato Na Matumizi

Kwa Upande Wake Mertidis Malivata (Mrs Chitimba) Nae Alikuwa Na Haya Yakuzungumza

Baada Ya Wanachama Kutoa Maoni Yao, Afisa Ushirika Kutoka Halmashauri Ya Wilaya Ya Mtwara Hamidu Ndago Akatoa Ufafanuzi Kuhusu Kanuni Za Ushirika Kuhusu Mkutano Huo Maalum.

Mwenyekiti Wa Chama Kidogo Cha Ushirika Amcos Naliendele Akasimama Kuwaomba Wanachama Kukubali Na Wapitishe Makisio Ya Mapato Na Matumizi Ya Msimu Ujao

Baada Ya Mwekiti Kuzungumza Ilibidi Lipitishwe Azimo La Mkutano Kuhusu Kukubali Au Kukataa Kupitisha Na Kusomewa Makisio Ya Matumizi Na Mapato Ya Msimu Ujao, Na Ikafikia Kwa Wanachama Hawataki, Hali Iliyopelekea Afisa Ushirika Kuhairisha Mkutano Mpaka Siku 21 Kuanzia Jana Ambapo Itakuwa Tarehe 09.07.2019 Ndipo Watakapofanya Mkutano Mkuu.

Baada Ya Hapo Gregory Millanzi Odillo Alizungumza Na Baadhi Ya Wanachama Wa Amcos Ya Naliendele Walitoa Maoni Yao Kuhusu Mkutano Mkuu Maalum Uliokuwa Na Agenda Ya Kupitisha Makisio Ya Mapato Na Matumizi.Jamii Fm Radio

Jamii Fm Radio

Location: Naliendele- Mtwara Frequency: 90.5 MHz Contact: jamiifmradio90.5@gmail.com mtukwaomedia@yahoo.co.uk +255712087580, +255782510474, +255685307828 Jamii FM Radio is a community radio that intends to operate its radio station pursuant to non commercial. The main objective is to raise discussion about issues that are important to the people in rural communities in the Mtwara and Lindi regions. Jamii FM Radio wants to offer people on the grassroots level a possibility to take part in the public debate about issues concerning their livelihoods, about alternative ways of development and through this process a chance to find the best possible solutions to the development of their local areas in order to advance democracy, human rights and good governance. Jamii fm ni kituo cha radio ya kijamii yenye lengo la redio kusaidia kupaza sauti za wanajamii hasa waishio vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa maendeleo kupitia majadiliano. Jamii Fm Radio inasaidia wananchi kuibua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa, kuhusu aisha yao, maendeleo yao, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. KARIBU SANA MTWARA-TANZANIA WELCOME MTWARA-TANZANIA

Leave a Reply