WENYE MAHITAJI MAALUMU WALILIA MIKOPO YA BIASHARA

Watu wenye mahitaji maalum wamezungumza na Jamii FM Radio Mtwara wameeleza changamoto wanazokumbana nazo katika maisha yao ya kila siku hivyo kushindwa kuchukua mkopo kwa ajili ya yakufanyia biashara ambazo zitawakwamua kimaisha.

Fatuma Samri ni mlemavu wa macho yeye anaeleza changamoto anazokumbana nazo ambazo ni pamoja kutopewa kipaumbele katika kutumia usafiri hasa daladala, kupata huduma za Afya, kusomesha watoto na kupata huduma za kijamii.

Ameiomba serikali iwasaidie katika kuhakikisha wanasomesha watoto na kupata huduma za afya kwa kuomba kupewa kipaumbele katika kumiliki viwanja vya kujenga nyumba.

Kwa upande wa NGO’s zinasaidia watu wenye mahitaji maalum, Jackline mpunjo yeye anaeleza kuhusu namna wanavyowasidia watu wenye mahitaji maalum wao kama shirika la SDA Wameleza namna ya kusaidia kuwasomesha vijana wenye mahitaji maalum ambao wanasoma kwenye chuo cha Veta Mtwara.

Na kwa upande wa serikali kupitia kwa Kaimu Afisa Maendeleo Halmashauri amethibitisha uwepo wa mikopo dhidi ya walemavu au watu wenye mahitaji maalum pamoja nameelezea kuhusu changamoto zilizopo katika utoaji wa mikopo dhidi ya walemavu.
SIKILIZA HAPA

Jamii Fm Radio

Jamii Fm Radio

Location: Naliendele- Mtwara Frequency: 90.5 MHz Contact: jamiifmradio90.5@gmail.com mtukwaomedia@yahoo.co.uk +255712087580, +255782510474, +255685307828 Jamii FM Radio is a community radio that intends to operate its radio station pursuant to non commercial. The main objective is to raise discussion about issues that are important to the people in rural communities in the Mtwara and Lindi regions. Jamii FM Radio wants to offer people on the grassroots level a possibility to take part in the public debate about issues concerning their livelihoods, about alternative ways of development and through this process a chance to find the best possible solutions to the development of their local areas in order to advance democracy, human rights and good governance. Jamii fm ni kituo cha radio ya kijamii yenye lengo la redio kusaidia kupaza sauti za wanajamii hasa waishio vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa maendeleo kupitia majadiliano. Jamii Fm Radio inasaidia wananchi kuibua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili kuanzia ngazi ya kijiji hadi kitaifa, kuhusu aisha yao, maendeleo yao, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. KARIBU SANA MTWARA-TANZANIA WELCOME MTWARA-TANZANIA

Leave a Reply