MKUTANO WA WANATAM TAM SALAM KLUB.

Na Baraka Ole Maika.

Mkutano wa Chama Kongwe katika Ulingo wa Salaam kwenye Vyombo vya Habari Tanzania Tam Tam Salaam Klub unafanyika leo katika Ukumbi wa Triple A’ Jijini Arusha.

Mkutano huo unawakutanisha Watuma Salamu Wakongwe na Chipulizi kutoka Mkoa wa Arusha,Manyara,Kilimanjaro,Tanga,Singida,Tabora na Mikoa ya Jirani ikiwa na Lengo la kujadili Umoja,Ushirikiano na Nafasi ya Watuma Salaamu katika kuelimisha Jamii hasa katika Kipindi hiki cha Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 ‘2015.

Akizungumza na Orkonerei Radio Service,Rais wa Tam tam Salaam Klub Baba Ally Mbondey amesema kuwa Lengo Kuu la Mkutano wao huo ni Kujadili Mustakabali wa Watuma Salaamu na Jamii ya Watanzania katika kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.

Aidha Baba Ally Mbondey amewaasa Watuma Salaamu kuwa Makini wakati huu wa Kuelekea Uchaguzi Mkuu na Kutojiingiza katika Vitendo vitakavyohatarisha Amani na Utulivu Katika Jamii.

Baba Ally Mbondey pia ameasihi Watuma Salaam na Watanzania wote kujitokeza kwa Wingi siku ya Uchaguzi ili kuwachagua Viongozi Bora watakaowatetea na kuwaletea Maendeleo na Mabadiliko kwani Watanzania sasa wanahitahi Mabadiliko.

orkonerei

Location: Simanjiro-Manyara Frequency: 94.4 Mhz Contact: Tel: +255 787 507 854 or +255 769 712 961 Orkonerei Radio Servce(ORS Fm 94.4) ni Radio ya Jamii iliyoanzishwa na Taasisi ya Kijamii ya Ilaramatak Lorkonerei(Institute for Orkonerei Pastoralists Advancement-IOPA) katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara June 2002 ikiwa na Lengo la Kutetea na Kuhamasisha Jamii ya Wafugaji katika Shughuli za Maendeleo na kuwajengea Ufahamu na Uelewa kupitia Upashanaji wa Habari katika nyanja ya Elimu,Afya,Mazingira,Jinsia,Uchumi,Mifugo,Kilimo,Uongozi na Utawala Bora.

Leave a Reply