Mkutano wa Chadema Terrat.

Na Mwasiti Iddi wa ORS FM.

Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Bw James Millya Kinyasi amefanya mkutano wa kunadi sera na kuomba kura kwa wananchi wa Kata ya Terrat Wilayani Simanjiro.

Katika mkutano huo Bw Millya amewaahidi wakazi wa Kata ya Terrat kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Wilaya ya Simanjiro atalishughulika tatizo la maji katika Kata hiyo na ambalo limekuwa tatizo sugu kwa wakazi wa Wilaya ya Simanjiro.

Aidha ameahidi ujenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ambayo itakuwa inamilikiwa na serikali ili kutoa fursa ya elimu kwa watoto wa jamii ya kifugaji na watanzania kwa ujumla.

Mkutano huo nusura uingie dosari baada ya Mtendaji wa Kata ya Terrat Bi Yenieli Kagonji kutoa tamko la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa muda waliopangiwa kufanya mkutano huo ulikwisha pita.

Kauli hiyo ilizua Tafrani kwa wafuasi wa chadema na Mgombea huyo hali iliopelekea mkutano huo kuchelewa kuanza japo ulikuja kuendelea na kukamilika kwa amani.

orkonerei

Location: Simanjiro-Manyara Frequency: 94.4 Mhz Contact: Tel: +255 787 507 854 or +255 769 712 961 Orkonerei Radio Servce(ORS Fm 94.4) ni Radio ya Jamii iliyoanzishwa na Taasisi ya Kijamii ya Ilaramatak Lorkonerei(Institute for Orkonerei Pastoralists Advancement-IOPA) katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara June 2002 ikiwa na Lengo la Kutetea na Kuhamasisha Jamii ya Wafugaji katika Shughuli za Maendeleo na kuwajengea Ufahamu na Uelewa kupitia Upashanaji wa Habari katika nyanja ya Elimu,Afya,Mazingira,Jinsia,Uchumi,Mifugo,Kilimo,Uongozi na Utawala Bora.

Leave a Reply