New Bulletin

23 September 2015
Baadhi ya wanasiasa wamekuwa na maoni hasi kufuatia utafiti wa kampeni za uchaguzi uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la TWAWEZA wakisema kuwa takwimu hizo siyo sahahi.
Katibu wa Baraza la Vijana Taifa wa chama cha African Democratic Alliance zamani kikiitwa TADEA Askofu MARK DIGANYEKA amesema matokeo hayo yamekuwa na utata kutokana na hamasa kubwa ya wananchi kuvutiwa na vyama vya upinzani.
Pia amesema sampuli iliyotumika kuhoji watu elfu 1 na 800 wakati Tanzania ina raia milioni 45 hakuna uwiano wa kiutafiti.
Kwa mujibu wa Taasisi ya TWAWEZA, takwimu za zimebaini kuwa CCM itashinda kwa asilimia 65, Chama Cha Demokrasia asilimia 25 na vyama vingine kwa asilimia 7.

End-

23 September 2015
Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania TMF umekusudia kuanzisha upya mpango wa kuwezesha upatikanaji wa habari zenye maslahi makubwa ya taifa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na wazalishaji vipindi ili kuongeza habari za ndani.
Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Ernest Sungura amesema mpango huo utasaidia vyombo vya habari kutimiza wajibu wa kisheria kwa maagizo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA ya asilimia 60 ya vipindi vinavyohusu masuala ya ndani.
Baadhi ya vyombo vya habari vinatangaza vipindi vingi kutoka nje ya nchi huku masuala ya ndani yakipewa nafasi kidogo tofauti na kuwakosesha wananchi habari zinazowahusu kwa maendeleo ya jamii zao.

End-

23 September 2015
Mtandao wa wanahabari watoto wamekutana na wanasiasa wa kada mbalimbali kuzungumzia masuala muhimu yanayopaswa kujumuishwa katika ilani za uchaguzi.
Watoto hao wamehoji juu ya ushirikishwaji katika ngazi za familia, shuleni na ngazi za uongozi serikalini.
Mtoto RATIFU HAJI NKAME kutoka shule ya sekondari RUANGWA mkoani Lindi amesema kuna na nafasi ndogo kwa watoto kufikisha mawazo yao ili kusaidia maamuzi yanayofanywa katika jamii.
Nae Afisa Tawala Msaidizi wa Makao Makuu ya ofisi ndogo ya CCM mkoani Dar es Salaam Bibi MWAJUMA NYAMKA, ameahidi kuwa endapo chama chake kitaingia madarakani watashughulikia suala hilo.

End-

23 September

Naibu Katibu mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika RAPHAEL DULUTI
Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya wakulima kwa kuhakikisha
Mbegu zinazosambazwa zinakuwa na ubora ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula.

Bwana DULUTI amesema mjini Morogoro wakati wa uzinduzi wa wa Bodi ya Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu TOSCI, kuwa serikali itashirikiana na taasisi nyingine za mbegu ili kufikia ubora wa uzalishaji.

Naye Mkurugenzi wa TAasisi ya mbegu ya TOSCI Dokta HAMIS MTWAENZI, amesema wako mbioni kujenga maabara za kisasa ili kuwezesha mpango huo wa mbegu bora.

End-

mlimani

mlimani

Location: Journalism street off Ally Hassan Mwinyi Rd, Kinondoni Dar es Salaam Frequency: 106.5 MHz Contact: P. O Box 4067, Dar es Salaam Email (Official) mlimani.media@udsm.ac.tz Editor: pdandi22@gmail.com This Radio Station is owned by School of Journalism and Mass Communication of University of Dar es Salaam. Its role is to train students who pursue in Journalism, Mass Communication and Public Relation and Advertising courses offered by the University of Dar es Salaam. Also it serves students from other universities and colleges both local and international. Like other media, Mlimani Radio also serves the society as one of community radios with the aims of informing, educating, entertaining and advertising. Mostly its run by students under supervision of three skilled, educated and experienced journalists -- Redio Mlimani inamilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, iko katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma. Kijiografia, kituo hiki kiko Mikocheni, mtaa wa Journalism kutokea barabara ya Ally Hassan Mwinyi (Makumbusho). Kituo hiki kinatoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi. Pia kinatoa huduma za habari kwa jamii na ushauri katika fani za Uandishi wa Habari, Mawasiliano, uhusiano na Matangazo.

Leave a Reply