News Story

29 September 2015

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ametoa onyo kwa wanasiasa wanaoshindwa kunadi sera zao badala yake kutumia muda mwingi kujadili watu.

Jaji Lubuva amesema kuacha kuzungumzia sera ni kosa na kwamba kwa mujibu wa Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015, wanasiasa hao wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Pia amekemea matumizi ya lugha mbaya zinazodhalilisha baadhi ya wagombea na kusema kuwa hali hiyo inaweza kuvuruga amani.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema hakutakuwa na wizi wa kura, na kwamba anayejua mbinu za kuiba kura atoe taarifa kwa tume hiyo ili iweze kuchukua hatua.

End-

mlimani

mlimani

Location: Journalism street off Ally Hassan Mwinyi Rd, Kinondoni Dar es Salaam Frequency: 106.5 MHz Contact: P. O Box 4067, Dar es Salaam Email (Official) mlimani.media@udsm.ac.tz Editor: pdandi22@gmail.com This Radio Station is owned by School of Journalism and Mass Communication of University of Dar es Salaam. Its role is to train students who pursue in Journalism, Mass Communication and Public Relation and Advertising courses offered by the University of Dar es Salaam. Also it serves students from other universities and colleges both local and international. Like other media, Mlimani Radio also serves the society as one of community radios with the aims of informing, educating, entertaining and advertising. Mostly its run by students under supervision of three skilled, educated and experienced journalists -- Redio Mlimani inamilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, iko katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma. Kijiografia, kituo hiki kiko Mikocheni, mtaa wa Journalism kutokea barabara ya Ally Hassan Mwinyi (Makumbusho). Kituo hiki kinatoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi. Pia kinatoa huduma za habari kwa jamii na ushauri katika fani za Uandishi wa Habari, Mawasiliano, uhusiano na Matangazo.

Leave a Reply