News

8 OKTOBA

Watafiti wa magonjwa ya binadamu, watunga sera, watoa huduma za afya na wadau wengine wanatarajia kukutana wiki ijayo jijini Dar es Salaam katika kongamano kubwa la masuala ya afya.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utatifi wa Magonjwa ya Binadamu NIMR Dokta MWELE MALECHELA, amesema siku hiyo pia itatumika kuzindua maadhimisho ya 35 ya Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania.

Mada kuu itakuwa ni uimarishaji wa afya na hali bora ya maisha kupitia tafiti zenye ubunifu na mpango wa kukabiliana na ongezeko la mseto wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukizwa barani Afrika.

End-

8 OKTOBA

Watu wenye ulemavu wamesema uchaguzi wa mwaka huu umeendelea kuwatenga kama chaguzi nyingine zilizopita kwa kushindwa kuwapa fursa nyingi za kugombea nafasi mbalimbali.

Wakiongea wakati wa kongamano lililofanyika jijini Dar es Saalam na kushirikisha wadau kutoka mikoani, watu hao wenye ulemavu wamesema vyama vingi vya siasa haviwapi nafasi watu wenye ulemavu kwa kuwa hata katiba zao hazitoi kipaumbele kuhusu jamii hiyo.

Hata hivyo wamekiri kuanza kuwa na mwamko na siasa, na kwamba wataendelea kupigania haki zao za kiraria kupitia vyama vyao kwa kuwa na sauti moja ya kutetea haki zao.

End- dsm

mlimani

mlimani

Location: Journalism street off Ally Hassan Mwinyi Rd, Kinondoni Dar es Salaam Frequency: 106.5 MHz Contact: P. O Box 4067, Dar es Salaam Email (Official) mlimani.media@udsm.ac.tz Editor: pdandi22@gmail.com This Radio Station is owned by School of Journalism and Mass Communication of University of Dar es Salaam. Its role is to train students who pursue in Journalism, Mass Communication and Public Relation and Advertising courses offered by the University of Dar es Salaam. Also it serves students from other universities and colleges both local and international. Like other media, Mlimani Radio also serves the society as one of community radios with the aims of informing, educating, entertaining and advertising. Mostly its run by students under supervision of three skilled, educated and experienced journalists -- Redio Mlimani inamilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, iko katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma. Kijiografia, kituo hiki kiko Mikocheni, mtaa wa Journalism kutokea barabara ya Ally Hassan Mwinyi (Makumbusho). Kituo hiki kinatoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi. Pia kinatoa huduma za habari kwa jamii na ushauri katika fani za Uandishi wa Habari, Mawasiliano, uhusiano na Matangazo.

Leave a Reply