
Msimamizi na muandaaji wa vipindi Radio Pambazuko Henry Mwakifuna akielezea changamoto za kimtandao kwa wakazi wa vijijini wakati wa mafunzo ya mtandao kwa radio jamii katika ofisi za MISA – TAN
Msimamizi na muandaaji wa vipindi vya radio Pambazuko Henry mwakifuna aelezea changamoto za kimtandao hasa kwa wakazi wa vijijini mkoani Mbeya alipo hojiwa wakati wa mafunzo ya matumizi ya mtandao kwa vituo vya radio za jamii. Mwakifuna asisitiza kuwa kwa wakazi wa mijini imekua rahisi kuchangia wakiwa wanasikiliza radio kwa njia ya mtandao hasa kwa kupitia mitandao ya kijamii, lakini hali ni tofauti kwa wakazi wa vijijini ambao wengi wao hawamiliki simu za mtandao na hivyo kuwawia vigumu kuchangia kwa kupitia mitandao ya kijamii…