Karibu katika Jukwaa huru la Habari,Vipindi na Maelezo kutoka Radio za Jamii Tanzania,Mimi ni Baraka Ole Maika kutoka Orkonerei Radio Service,Simanjiro-Manyara.

Na Baraka Ole Maika:

Orkonerei Fm Radio Service(ORS Fm 94.4) ni Radio ya Jamii iliyoanzishwa June 2002 na Taasisi ya Kijamii ya Ilaramatak Loorkonerei iliyopo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.

Lengo la Radio hii ni Kuelimisha,Kuhabarisha na Kuburudisha Jamii kupitia Vipindi mbali mbali vya Elimu na Habari ikiwa ni pamoja na kutafsiri Vipindi na Habari kwa Lugha ya Kimasai kupitia Kibali Maalum kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA).

Kwa Miaka 13 sasa tunajivunia Ufanisi na Uweledi uliotukuka katika Tasnia ya Habari ndani ya Jamii tunayoitumikia katika Mkoa wa Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga.

Kupitia Vipindi vya Radio yetu tumeshuhudia Mabadiliko Chanya ya Maendeleo,Elimu na Uchumi katika Jamii ya Wafugaji na Watanzania kwa ujumla katika nyanja ya Elimu,Afya,Mazingira,Kilimo,Ufugaji,Utamaduni,Uongozi na Utawala Bora,nk.

Orkonerei Radio Service(ORS Fm 94.4 Mhz)”Sauti ya Wachungi”

orkonerei

Location: Simanjiro-Manyara Frequency: 94.4 Mhz Contact: Tel: +255 787 507 854 or +255 769 712 961 Orkonerei Radio Servce(ORS Fm 94.4) ni Radio ya Jamii iliyoanzishwa na Taasisi ya Kijamii ya Ilaramatak Lorkonerei(Institute for Orkonerei Pastoralists Advancement-IOPA) katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara June 2002 ikiwa na Lengo la Kutetea na Kuhamasisha Jamii ya Wafugaji katika Shughuli za Maendeleo na kuwajengea Ufahamu na Uelewa kupitia Upashanaji wa Habari katika nyanja ya Elimu,Afya,Mazingira,Jinsia,Uchumi,Mifugo,Kilimo,Uongozi na Utawala Bora.

One Comment

Leave a Reply